Tuesday, June 19, 2012

Mwananyika aka Drogba wa Mloka (Selous GR)

Ukifika kijiji cha Mloka (kijiji cha mwisho kabla ya kuingia Selous GR ukasikia watu wanamzungumzia Drogba basi kuna uwezekano mkubwa wakawa wanamzungumzia Drogba wao anayeonekana kushoto na sio yule ambaye wewe umemzoea. Huyu jamaa wengi hata jina lake kamili hawalijui lakini ni mmoja kati ya watu maarufu sana kijiji hapo na hususan kwa wadau wa utalii ambao hupeleka wageni kwenye pori la akiba la Selous kupitia lango la Mtemere (lango unaloingilia Selous GR ukitokea kijiji cha Mloka). Shughuli zake ni kupeleka wageni katika safari za matembezi maeneo pembezoni mwa mpaka wa Selous GR na kijiji cha Mloka. Kwa kuwa pori la Selous halina uzio, wanyama hutoka nje na kuzunguka vijijini na maeneo karibu hivyo kutoa fursa kwa wageni kufanya walking safari ambazo huwaleta karibu na wanyama wa porini.  Wanyama kama Tembo, Swala mbalimbali, Nyati, Viboko, Twiga na kadhalika huweza kuonekana maeneo ambayo Drogba hupiga misele na wageni wake.
Mara nyingi anapokuwa anafanya safari hizi, huwa anaambatana na askari mwenye silaha. Kwenye picha hii askari yupo nyuma ya drogba. Yeye alianza kwa kujiita Mwananyika, lakini wananchi waliamua kumpa jina la Drogba kwa madai ya kuwa anafanana na Drogba anayeputa ndinga huko majuu. 

Ieleweke ya kwamba kwa mgeni ambaye atafanya walking safari nje ya hifadhi, wadau kama akina Drogba na walinzi wa hoteli/campsite husika wanaweza kumsindikiza. Kwa yule ambaye anataka kufanya walking safari ndani ya hifadhi au pori la akiba ni lazima asindikizwe na askari wa wanyama pori. katika situation zote, wote huwa wanakuwa na silaha kwa lengo la kujihami. Matumizi ya silaha kwa lengo la kumuu mnyama huwa ni option ya mwisho baada ya mbinu zote kuepusha hatari kugonga mwamba. Shukran ya picha kwa Mdau Rajab Idd wa Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Post a Comment