Tuesday, June 19, 2012

Zanzibar (Unguja) mashambani ndio huku

Si ajabu ukiwasikia wenyeji wako kule Unguja (Zanzibar) wakizungumzia maeneo ya mashambani na hata wengine wakikuambia kuwa huko uendako ni mashambani. Kwa wenyeji, wanaposema mashambani ni maeneo ambayo yapo mbali na Unguja mjini, Mji Mkongwe na maeneo mengine karibu napo. Mashambani ni maeneo ambako ndipo mahoteli mengi ya kitalii yalipojengwa. na Ndipo uwekezaji mkubwa ktk sekta ya utalii unapoendelea. Nikilinganisha na huku bara ni sawa na mtu akisema unaenda Morogoro, Tanga au Dodoma. Unapokuwa unatembea maeneo hayo yanayoitwa mashambani unaweza kupata picha tofuati na ile uliyozoea ya eneo lijulikanalo kama shambani. Kwani 'mashambani' ya Visiwani mambo yamekaa kimjini mjini na huduma muhimu za mjini zinapatikana pia. Picha ya juu ni maeneo ya Pwani Mchangani huko Kaskazini-Mashariki ya Kisiwa cha Unguja. hapo tulikuwa tunatoka Maeneo ya Kiwengwa kuelekea Mji mkongwe na kisha Airport. Ni Umbali wa kilometa  45. mwendo wa kama dakika 50 hivi mpaka kufika Mji mkongwe. Na hapo (Pwani Mchangani) sio kule juu kaskazini kabisa - Nungwi. Bado kuna mwendo wa Kilometa kadhaa mpaka kufika Nungwi.

Wakati mwingine unaweza ukadhani upo Mkoa wa Kilimanjaro au Kagera kwa jinsi baadhi ya maeneo yalivyojaa migomba kila upande wa barabara.

Eneo hili kulikuwa na shamba kubwa la mpunga pande zote mbili za barabara.


hapa ni maeneo ya Bandamaji.

Safari inaendelea, jambo moja lililonifurahisha ni kwamba safari yetu yote tulikuwa kwenye barabara iliyojengwa kwa Lami. Hili ni jambo la kuipongeza SMZ kwani hata zile sehemu chache ambazo kulikuwa na hitilafu, mkandarasi alikuwa eneo la kazi akifanya marekebisho.


No comments:

Post a Comment