Monday, June 18, 2012

Mambo ya Whirlwind Aviation

Helikopta hii inamilikiwa na kampuni ya Whirlwind Aviation Tanzania yenye makazi yake Jiji Dar. Helikopta hii ilikuwa jijini Arusha ktk maonesho ya utalii ya Karibu 2012. Walitoa fursa kwa wadau wachache kuzungushwa juu ya viwanja vya maonesho na maeneo yanayovizunguka. Kampuni hii ipo kwenye mkakati wa kuleta nchini helikopta 5 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu. Lengo likiwa ni kuzitawanya sehemu mbalimbali za nchi yetu ili ziweze kutumika kwa ajili ya usafiri wa kawaida au katika dharura na majanga mbalimbali pale inapofaa. Sasa hivi ngome yao kubwa imekuwa ni jiji la Dar Es Salaam. Picha juu ni mimi nikila pozi la picha kabla ya kupanda helikopta hiyo, pembeni yangu aliyenifungulia mlango ni Greg ambaye yeye ni paramedic wa Whirlwind Aviation Tanzania

Captain Neels akipasha moto mchuma kabla ya kuanza kupiga misele  
Abiria tukiwa tayari kwa safari yetu fupi.


Ni jambo la lazima kwa abiri kuvaa hizo headphones wakati wote wa safari. Helikopta ina kelele sana na ukiaa bila hizi unaweza poteza uwezo wako wa kusikia au kupata shida mara baada ya safari yako. Ukivaa hizo headphones sambamba na microphone yake abiria mnaweza kuzungumza na kusikilizana - ni ajabu lakini kweli.

Picha baada ya safari.

Mchuma wenyewe ulikuwa umepaki nje ya uwanja wa maonesho lakini ndani ya viwanja vya magereza nje kidogo ya jiji la Arusha. Hii safari itabaki kuwa ndio mara yangu ya kwanza kupanda Helikopta.

No comments:

Post a Comment