Monday, June 4, 2012

Bwawa la Viboko - Mikumi National Park

Bwawa La Viboko ndani ya Hifadhi ya taifa ya Mikumi ni moja ya vivutio ambacho wageni wanaoitembelea Mikumi lazima wapite. Hapa ni moja ya maeneo ndani ya hifadhi ambapo Mgeni anaruhusiwa kushuka toka kwenye gari na kutembea kidogo (japo sio mbali na lilipo gari). Eneo hili lina umuhimu hasa wakati wa kiangazi kwani ni moja ya chanzo muhimu cha maji kwa wanyama. wanyama wengi huja hapa kunywa maji hali ambayo huwafanya sharubu na wanyama wengine wala nyama kuja kutega mitego yao ktk mapito ambayo yanakuja kwenye hili bwawa au pembezoni mwa bwawa lenyewe.

Mdau Rajab Idd wa Wildness Safaris Tanzania ameturushia taswira hii toka Mikumi NP ambayo imepigwa hivi karibuni pembezoni mwa bwawa la Viboko.
********
Wadau na wapenzi wa Blog ya TembeaTz mnaweza nanyi pia kutuma picha na story za shughuli zenu (binafsi au kampuni) ili zirushwe kwenye Tembea Tanzania blog kwa kupitia email ya tembeatz@gmail.com. Hili ni jukwaa la kupashana habari mbalimbali na kufahamishana nani anafanya nini na nini kipo wapi na kinapatikana vipi. Karibuni

KK
tembeatz@gmail.com

No comments:

Post a Comment