Saturday, May 12, 2012

Tafiti ni muhimu.... Mikumi national park

Jana mida ya jioni nilikutana na hawa jamaa wakiwa ndani kabisa ya hifadhi ya taifa ya mikumi wakiwa ktk hali iliyojithihirisha wapo ktk shughuli za ki utafiti. sambamba nao kulikuwa na askari wa wahifadhi wanyama pori ambao walikuwa na silaha. Pichani ni baadhi yao, kundi lingine lilikuwa mbali kidogo na barabara.

Uhifadhi ni jambo endelevu hivyo linahitaji tafiti za mara kwa mara ili kuona kama jitihada zinazaa matunda au zinahitaji kuongezewa nguvu mpya. Wanafunzi na hata wahitimu wa masomo ya sekta mbalimbali za uhifadhi huwa na habari nyingi za kusisimua kutokana na changamoto au hatari wanazopambana nazo wanapokuwa kwenye utafiti au ktk kazi zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment