Friday, May 4, 2012

Alikuwa anaenda Kutua Uwanja wa Ndege wa Arusha

 Viwanja vya Magereza vipo pembezoni mwa Uwanja wa ndege wa Ausha, Sehemu ambayo maonyesho ya Karibu fair hufanyika ipo usawa wa njia ya kurukia na kutua ndege. Si jambo la ajabu unapokuwa hapo ukasikia kelele za ndege zikipita kwa karibu wakati zikielekea kutua ktk uwanja huo kama ambavyo kamera ya TembeaTz ilivyoinasa ndege hii hapa mwaka jana.
Ikizidi kukaribia eneo la maonesho

Hapo Rubani akielekea kutua. majengo ya uwanja wa ndege ni yale yanayoonekana upande wa kulia wakati barabara ya kuruka na kutua ipo ktk usawa inapoelekea ndege. Uwanja huu upo njia inayoelekea Babati na kwengineko. (Picha zote toka maktaba ya TembeaTz)

1 comment: