Wednesday, May 30, 2012

Safari ya Kuupanda Mlima Meru

 RA safaris Mount Meru Trekking
Ni Kundi la wageni waliofanya safari yao ya kuupanda Mlima Meru. Safari za kuupanda Mlima Meru huanzia ndani ya Arusha National park. Kimsingi, Mlima Meru ni sehemu ya Arusha National Park. safari yao ilikuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya RA Safaris. Njia hii hujulikana kama Momella Route.

 RA safaris Mount Meru Trekking
 Safari inaendelea, Mapumziko ya hapa na pale ni muhimu ili kuweza kutimiza lengo la kufika kileleni.

 RA safaris Mount Meru Trekking

 RA safaris Mount Meru Trekking
 Kwakuwa hatua za awali za safari (na baadae mwishoni) huwa zinapita ndani ya hifadhi yenye wanyama pori, sehemu hii wapanda mlima huwa wanasindikizwa na ranger mwenye silaha. Yeye jukumu lake ni kuhakikisha wapandaji hawakutani na hatari zozote zitokanazo na wanyama wa porini waliopo eneo hilo. Huu mpango upo Mlima Meru tu, kwa Mlima Kilimanjaro wapandaji wanakuwa na msindikizaji wao tu.

 RA safaris Mount Meru Trekking
Wadau wa RA Safaris na Askari wa Wanyama pori (aka Ranger) wakipozi kupata picha wakiwa safarini kuupanda Mlima Meru. 

 RA safaris Mount Meru Trekking
moja ya Kumbukumbu za kuwa Mlima Meru ni mlima uliotokana na milipuko ya Lava miaka lukuki iliyopita bado inaonekana vyema kwa wapandaji wanapokaribia kufika kileleni. Bofya hapa kwa taarifa zaidi kuhusu ruti ya kupandia Mlima Meru na vituo vyake. Picha zote kwa mdau Zeph wa RA Safaris

No comments:

Post a Comment