Thursday, May 3, 2012

Muonekano wa Serengeti tokea Naabi Hill Gate - Serengeti NP

Naabi Hill ni mlima ambao upo ndani ya Hifadhi ya Serengeti kwenye barabara kuu inayounganisha Serengeti na eneo la hifadhi la Ngorongoro na maeneo mengineyo. Naabi ndipo kuna geti la kuingilia rasmi ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Hapa ndio vibali vya kuingia rasmi ndani ya Hifadhi vinapotolewa kwa wale wanaoingia na pia kwa wale wanaotoka, ndio sehemu vibali vyao vinapokaguliwa na kuhakikiwa. Natumia neno 'rasmi' kuondoa dhana ya kwamba hapa ni mpakanni. Mpaka baina ya Serengeti na Ngorongoro upo mbali kidogo (kabla ya kufika hapa) eneo ambalo wazee wa pori huliita Golini (bofya hapa kujikumbusha mtunduko uliopita kuhusu golini). mpaka unapofika Naabi tayari unakuwa umeshaingia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na unaweza ukawa umeshajionea wanyama kedekede ukiwa njiani kufika hapo tokea Golini.
Kama ilivyo  kwenye mageti mengine ya kuingilia kwenye Hifadhi, mgeni anakuwa na fursa ya kushuka, kutembea, kujinyoosha na hata kula chakula alichobeba. Eneo hili kuna 'vimbweta' vya kupatia msosi kwa wageni. Mbali na hayo yote, kuna baadhi ya sehemu zinatoa fursa nzuri ya kuuona uwanda wa nyasi wa Serengeti tokea kwenye kilima hiki cha Naabi.

Hapa ni pale ambapo mnakuwa mnaindelea na safari yenu kuelekea Maeneo mengine ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. (picha zote toka Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment