Thursday, March 8, 2012

mambo ya Singita - Grumeti Reserve

Kama ni ubunifu na kisha kuthubutu basi binafsi nawavulia kofia kampuni ya Singita kwa kubuni aina hii ya safari ambayo mgeni anatembea ndani ya hifadhi na kuangalia wanyama akiwa kwenye mgongo wa Farasi. Hii sio maigizo wala muvi bali ni mpango wa kweli ambao upo hapa Tanzania ktk pori la akiba la Grumeti linalosimamiwa na kuendeshwa na kampuni ya Singita. Pori hili lipo sambamba kwenye ecosystem ya Serengeti kwenye eneo ambamo migration hupita pia. Picha juu ni wageni wawili wakitembea ndani ya pori la Grumeti wakiwa kwenye migongo ya farasi sambamba na guide wao. Yataka moyo lakini pia wapo wenye huo moyo.

kama ilivyo kwenye safari za magari, muda wa lunch ukifika wageni wanawaegesha farasi pembeni na kisha wao kupata chakula chao na kupumzika kabla ya kuendelea na mizunguko.
Bofya hapa kupata dondoo zaidi kuhusu namna hii ya kutembelea hifadhi ya Grumeti
(picha zote toka - www.singita.com)

3 comments:

  1. du! imenishtua kidogo lkn nimekubali. asante sana kutuhabarisha kweli huu ni utalii wa aina yake Hongera kwa Tanzania pia.

    ReplyDelete
  2. ki ukweli Grumeti wanajua biashara, kwa hilo nawakubali, pia wanastandards nzuri. Lakini sijasikia kama wana bei za wa Tanzania(RESIDENT RATES).Maana gharama zao ziko juu kwa m Tanzania wa kawaida.

    ReplyDelete