Wednesday, March 7, 2012

Utalii sio kwenye mbuga na hifadhi...

Kwenye jamii nako kuna mambo mengi unayoweza kujifunza na kukupa hamasa akilini mwako. Huku unaweza kuona na kujifunza ni namna gani jamii hizi zinakabilia na changamoto za maisha yao ya kila siku. Baadhi ya changamoto zao zinaweza zisiwe kama changamoto kwako lakini bado utakuwa na nafasi ya kujifunza mambo mengi mapya. Maisha yao ya kila siku na shughuli zao za uzalishaji mali na kipato ni moja ya mambo ambayo yanaweza kukuvutia na wakati mwingine ukabakia mdomo wazi.


Uelewa na ufahamu wao kuhusu mazingira wanayoishi na jinsi wanavyoweza kuishi pamoja ni nyanja nyingine yenye mafunzo mazuri kwako ukiwatembelea. Hii si kwa wageni wanaotoka nje ya nchi kwani hata sisi Wa hapa nyumbani pia tuna mengi ya kujifunza. Picha juu ni wageni waliokuwa na Mdau Tom walipo simama kwenye moja ya vijiji vilivyopo pembezoni mwa barabara iendayo Selous. Wageni hawa walistaajabishwa na matumizi ya zana mbalimbali za asili ktk kutengeneza madawati na vifaa vingine vya samani.

2 comments:

 1. jamani this is better creation and led tanzania to be creative in and out of africa nimeipenda sana hii blog
  me wambura mwikwabe
  +255 754766910
  babuwambura@gmail.com
  babuwambura@yahoo.com

  ReplyDelete
 2. Shukran sana babu Wambura kwa comments na contact zako. Karibu sana na endelea kuwa mdau wa TembeaTz blog. mambo mazuri yanakuja

  ReplyDelete