Thursday, March 8, 2012

Kinaitwa kisiwa nyoka

Ukiwa njiani kuelekea kisiwa cha Mbudya utapita kisiwa hiki ambacho wazoefu tuliokuwa nao walitueleza kuwa kinaitwa Snake Island, kisiwa cha Nyoka. Ni kisiwa ambacho sehemu kubwa ya kingo zake zimezingukwa na mawe na kukifanya kutokuwa na mvuto kwa wageni wanaopendele pwani zenye mchanga mweupe.
Nilipodadisi kuhusu jina la kisiwa hiki nikadokezwa kuwa ni kweli kuna aina kadhaa za nyoka katika kisiwa hicho. Wamefikaje, wanaishije ni maswali ambayo ukiniuliza nitashindwa kukujibu sasa hivi lakini taarifa za uwepo wao nimewahi kuzisikia mara kadhaa.

No comments:

Post a Comment