Tuesday, March 13, 2012

Mambo ya Mbudya...

Mbudya ni Moja ya visiwa vilivyopo katika pwani ya Kaskazini mwa jiji la Dar Es Saalam, Maeneo ya Kunduchi. Ni eneo ambalo ni tengwa kwa lengo la kulinda na kuhifadhi viumbe wa baharini wanaopatikana eneo hilo. Hii haizuii wageni kwenda na kupumzika kisiwani hapo. Wadau wengi hivi sasa wamekuwa wakikitumia kisiwa hiki kama eneo la mpumziko ya weekend na siku nyingine za wiki huku wengine wakienda mbali hadi kupiga kambi ndani ya kisiwa - tented camping. Kipo chini ya Wizara ya Uvuvi (Sio Utalii na Maliasili). Kimsingi kuna njia moja kuu ya kuweza kufika hapo ambayo ni kwa njia ya Boti. Unaweza kwenda kwa boti binafsi au kwa kutumia boti 'za umma' ambazo zinafanya safari mara kwa mara katika siku tokea katika hoteli mbalimbali zilizopo kwenye pwani ya kunduchi. Huduma ya boti hizi ipo ktk hoteli za white sands na Jangwani Sea breeze. Ubao juu unakupa taarifa kadhaa za kuzingatia kama mgeni uwapo katika kisiwa cha mbudya.

Kuwa ktk eneo la kina kirefu kunamhakikishia mgeni wa kisiwa hiki fursa ya kupata maji ya kina kirefu muda wowote kwa yule ambae kuogelea ni sehemu ya starehe na mapumziko yake awapo ufukweni. Kina pWani nzuri yenye mchanga mweupe.

Maji yanapokuwa yamekupwa, pwani za kisiwa cha mbudya hutoa fursa kwa wageni kuafanya michezo kadha wa kadha kwenye mchanga. licha ya hili, maji yenye kina cha kutosha huwepo pia hata wakati wa maji kupwa (kina kifupi), tofauti na maeneo mengine ambako maji huwa yanakuwa kama hayapo kipindi hiki

huu ni upande mwingine unaojulikana kama Campsite. Kuna mwekezaji alipewa fursa ya kuanzisha na kuendesha campsite pembezoni mwa hapa, lakini inaelekea mipango haikuwa sawia na mategemeo hali iliyopelekea baadhi ya vitu kuachwa kama havina mwenyewe. Sasa hivi anayekuja hapa kisiwani yupo huru kupunga upepo upande huu. Pwani ya upande huu nayo ina mchanga mweupe na sehemu nzuri ya kuogelea pia. Kitu kimoja cha nyongeza kwa kisiwa cha Mbudya ni kwamba mgeni una uwezo wa kuleta vyakula na hata vinywaji vyako kama utapenda. Japo vinywaji baridi na hata vya moto vinapatikana.

huu ndio usafiri tulioutumia siku hii. Unafanya safari zake kati ya kisiwa cha Mbudya na Hotel ya White sands. Hapo nahodha alikuwa anauweka sawa tuanze kupanda na kurudi Mjini mida ya jioni.
Abiria wakijivuta kwenda kupanda boti tayari kwa safari ya kurudi. Wengi wetu tulikuwa tumeanzia safari ktk hoteli ya white sands. Unaweza kuwasiliana na Mdau Omary kupitia 0713202946 ili akupe mpango mzima wa jinsi ya kufika huko na gharama husika. hata hapa, wazawa tuna punguzo la bei kwenye kiingilio cha kisiwani.
(picha zote - maktaba ya TembeaTz)

5 comments: