Tuesday, March 13, 2012

Shughuli ya Selous hii...

Pori la akiba la Selous huwa na changamoto kibao hususan hali ya hewa ikibadilika na mvua kuanza kunyesha. Picha hizi ni ushahidi wa hali ilivyo sasa hivi baadhi ya sehemu/barabara ndani ya pori la akiba la Selous. Kama dereva au guide hana ma-ujanja mnaweza mkaweka kambi mahali pasipostahili.

Mara nyingi kipindi cha mvua kikianza, kuna baadhi ya sehemu ndani ya pori la Selous zinakuwa hazifikiki kutokana na changamoto za miundombinu. Yote kwa yote Mdau alifanikiwa katika safari na kuweza kuona vitu vizuri kibao ambvyo blog ya TembeaTz itakuwa inakudondoshea.
Shukran ya picha kwa mdau Tom wa Kima Adventures

No comments:

Post a Comment