Tuesday, March 13, 2012

Boat Safari ndani ya Selous Game Reserve

Kujaa maji ya mto Rufiji na mabwawa yake sio ndio mwisho wa safari za wageni. huu huwa ni mwanzo wa namna nyingine za kulitembelea pori hili na kujionea kilichopo huko. kwa kuwa kina cha maji kinaongezeka kina mahali, safari za kuangalia wanyama kwa njia ya boti huongezeka na kuvutia wengi kipindi hiki. Hii inatokana na ukweli kwamba baadhi ya maeneo ambako wanyama wanakuwepo kunakuwa hakufikiki kirahisi na mara nyingine wanyama wanaopendwa huwa wanakuwa pembezoni ya mto. Baadhi ya haya maeneo yanakuwa ni ardhi kavu kipindi cha kiangazi na kufikika kiurahisi kwa magari. Mvua ikinyesha na mto Rufiji ukijaa, habari hubadilika na kuwa tofauti.

haya ni makundi mawili tofauti ya wageni ambayo licha ya kutembelea pori la Selous kwa njia ya gari waliamua kutumia pia usafiri wa boti ndani ya hifadhi ili kujionea mengi mengineyo kwa njia hii.


(picha zote na mdau Tom wa Kima Adventure)

2 comments:

  1. Sikuwahi kutembelea hii blog ila kuanzia leo ntakuwa mdau wako,kuna vitu ambavyo najifunza na kujionea sehemu ambazo sijawahi kufika ila nashawishika!!

    ReplyDelete