Thursday, February 2, 2012

Hii ndio ilikuwa lunch yetu chini ya Mbuyu Mkubwa, Selous Game Reserve

Mdau Tom (kulia) akishuka na cooler box ambalo lilikuwa na lunch yenyewe na visindikiza lunch.
Hii ilikuwa ni kwenye ule Mbuyu mkubwa uliopo ndani ya pori la akiba la Selous. Kwa mbali nyuma utawaona twiga kadhaa wakiendelea na shughuli zao. Hili ni eneo ambalo mgeni anaruhusiwa kushuka kwenye gari kwa ajili ya kupata chakula au hata kujinyoosha. Ieleweke ya kwamba sehemu nyingine (ndani ya hifadhi au pori) mgeni mwenye kibali cha game drive haruhusiwi kushuka nje ya gari labda.


Hakuna kiti wala meza, unatumia utakachokuta kujisitiri. hili ni jambo la kuangaliwa kwani sehemu hizi zinahitaji huduma nyingine muhimu kwa mgeni ikiwemo meza na kiti. Picha juu ni mimi kushoto na mdau Tom upande wa kulia.

Hii ilikuwa ni mwezi oktoba mwaka 2011
[Maktaba ya TembeaTz]

3 comments:

  1. kaka amna hata ndovu kwenye hiyo cooler box? pametulia sana hapoo....km ngapi from dar?

    ReplyDelete
  2. ha ha ha.. Hilo la ndovu ni beyond the scope of this book!
    kuhusu umbali; toka Dar mpaka kwenye geti la Mtemere ni 250Km- Dar Kibiti 150km halafu Kibiti Mloka/Mtemere 100Km. kutoka geti la mtemere mpaka ulipo mbuyu huu ni kama 40Km hivi. Nadhani anony wa kwanza utaweza kupata picha ya umbali kwa maelezo hayo.

    ReplyDelete