Ni Uwanja mdogo wa ndege wa Mtemere uliopo pembezoni mwa geti la Mtemere, geti la kuingilia kwenye pori la akiba la Selous huko Mloka Rufiji. Ni uwanja ambao unatumika zaidi na ndege ndogo ambazo huleta wageni ukanda wa Mtemere. Selous kuna viwanja kama hivi kadha wa kadha vingiwe vikiwa chini ya usimamizi wa hotel ambazo ndio watumiaji wakuu. Picha hizi zilipigwa wakati wa kumalizia game walk ambapo tulikuwa tunarudi kwenye geti la mtemere ili tuendelee na mambo mengine. unayoiona kwenye picha ya juu ni njia ya kurukia na kutua ndege - runway - ya uwanja huu.
Mashirika kadhaa ya ndege ndogo yana safari za kila mara (scheduled) kwenda Selous kupitia kiwanja hiki. Coastal Air ni mojawapo.
Eneo la maegesho ya ndege wakati wa kushusha na kupakia abira.
Magari ya hoteli na makampuni mengine yakiwa pembe ya uwanja yakisubiri ndege ya coastal ili wapokee wageni wao. Coastal hupeleka ndege mara mbili kwa siku ktk kiwanja cha Mtemere. Ya kwanza hutua saa nne asubuhi na ya pili (mwisho) hufika majira ya saa kumi jioni. (picha - maktaba ya TembeaTz)
hi! wakuu? vp mbona kimya longtime? au ni kuzidiwa na majukumu?
ReplyDeletekwanza niwapongeze sana kwa blog hii kwa kweli mm binafsi hua natembea tanzania kupitia hapa kwenye blog hii najifunza mengi nisiyoyajua, kupotea kwenu kwa muda kumeninyong'onyeza sana make kila nikipita hapa kijiweni nakuta patupu duu!!!!
any way najua maisha yetu ya sasa ni mchakamchaka kama ule wa (mbweha wa selous)hahahaaa!!! kukosa muda wa kupost new topic sitawalaumu sana nawaelewa. tupo pamoja sana..... big up!!! na poleni kwa majukumu