Wednesday, January 4, 2012

Njia ya kuelekea Kifungilo Secondary, Lushoto

Mliosoma Kifungilo Secondary school (Girls) mnalikumbuka Daraja hili? sambamba na hilo la miti pembeni yake ambalo lililkuwa linatumika awali kabla ya kuboreshwa?
Katika moja ya siku nilizokuwa Lushoto, nilikuwa na ratiba ya kufanya matembezi ya miguu katika vijiji na maeneo mbalimbali ambayo yapo karibu na Hoteli tuliyofikia ya Mullers Mountain Lodge. Moja ya eneo tulilopanga kulitembelea ilikuwa ni maporomoko ya maji ya mto Mvuezi ambayo yapo karibu na ilipo Shule ya sekondari ya wasichana ya Kifungilo ya huko Lushoto.

Kufika yalipo maporomoka hayo (ukitokea Mullers) unakuja mpaka lilipo Daraja hili na baada ya kufika hapa unaachana na barabara na kuanza kuambaa na mto mpaka yalipo.

Nilijulishwa na guide wangu siku hii ya kwamba daraja la Zege lilijengwa miaka ya tisini wakati awali daraja la mbao/magogo ndio lilikuwa likitumika. Mliosoma na kwenda kutembelea ndugu jamaa na marafiki mnalikumbuka Daraja hili? Linaleta kumbukumbu zipi?

1 comment:

  1. KK hapo namkumbuka dada yangu, japokuwa mimi sikuwahi kufika kifungulo. ilikuwa shule prestigious sana miaka ya 80 na 90. natumai bado ni shule ya ngufu

    ReplyDelete