Wednesday, January 4, 2012

Vinyonga wa Milima ya Usambara

Milima ya Usambara inaelezwa ya kuwa ina idadi kubwa ya wanyama aina ya Vinyonga. Wakiwa wa kila aina. Ukiwa huku huna haja ya kwenda mbali ili kuwaona. Palipo na kichaka au miti hususan ile ya matunda na mazao mengine, Vinyonga wanakuwa karibu napo.

Kwakuwa wapo nje ya eneo la uhifadhi unaweza kuwasogelea na kuwashika mkononi.

Huyu tulimkuta akiwa anaota jua kwenya tawi la Mtunda Damu (Red Plums). Nilipokuwa Lushoto ndio nilipata fursa ya kujua ya kwamba Red plums huwa za Kijani awali kama unavyoziona ktk picha juu. Zinapokaribia kuiva ndio hubadilika rangi na kuwa nyekundu kama vile ambavyo wengi wetu tumezoea kuziona pale Mombo, masokoni au mitaani.

No comments:

Post a Comment