Tuesday, January 3, 2012

Ni Tunda moja ila walaji ndio tofauti....

Picha juu inaonyesha jinsi utafauti wa mifumo ya ulaji na hasa hasa mmeng'enyo wa chakula inavyotofautiana kati ya mnyama mmoja hadi mwingine. Juu kulia ni tunda la mti wa Mkochi (upo kama palm tree hivi) ambalo halijaliwa na mnyama yoyote. Juu kushoto ni Tunda ambalo kwa mujibu wa guide, tunda hili lililiwa na Tembo wakati la chini alitueleza ya kuwa limeliwa na Ngedere.

Ukiangalia vyema, hususan haya matunda yaliyoliwa utabaini ya kwamba kila mnyama anautaratibu wake wa kula. Tembo kwa kuwa ana mdomo mkubwa na mfumo mkubwa wa kumeng'enya chakula ana uwezo wa kulimeza tunda zima zima na kulitupia tumboni. Ngedere yeye hulazimika kulimega mega tunda hilo ili kuweza kupata sehemu laini za nje ambazo mfumo wake zinaweza kumudu.

Uwapo porini hata mabaki ya chakula cha wanyama yanaweza kuwa ni darasa na maarifa muhimu kwako kujua. hivi ni vijimambo unavyoweza kunufaika navyo unapofanya walking safari. Hii ilikuwa ni ndani ya pori la akiba Selous

No comments:

Post a Comment