Ndege hutofautiana kwa namna na jinsi ambavyo hujenga na kutumia viota vya. Wapo ambao hutengeneza viota vyao kwa kutumia majani huku wengine wakitengeneza vyao kwa kutumia bidhaa mbalimbali ambazo zinapatikana ktk maeneo waliomo. Picha juu ni viota vya weaver birds (ndege mnana) ambavyo vimejengwa juu ya mti. Hapo kuna viota kadha wa kadha na baadhi ni viota vya kuzuga. Weaver birds hutengeneza viota vingi ili kuwachanganya maadui zao. Huishia kutumia viota vichache. Kiota ambacho ndege mwenyewe huamua kukaa huwa na milango miwilli ili kumwezesha kumtoroka mvamizi.
Hiki ni cha Hammerkop aka Fundi Chuma. Yeye huokota chochote kinachompendeza machoni mwake na kwenda kukutumia ktk ujenzi wa kiota chake. ukikichambua hicho kiota utakutana na kila ghasia ya takataka unayoijua. Zipo story za baadhi ya viota kukutwa na hata mifupa ya wanyama kama sehemu ya vifaa vya ujenzi. Ktk jamii mbalimbali kumekuwa na dhana tofauti kuhusiana na ndege huyu na pia kiota chake (sipendi kuingia sana nyanja hizo). Fundi chuma huacha mlango ambao wazoefu waliniamba mara nyingi sana unakuwa unaelekea upande ulio na chanzo cha maji. Kwa kiota hicho, upande ambako mlango unapoelekea ndipo ulipo mto Rufiji. Anapomaliza kutamia mayai yake na watoto kukua huachana nacho na kuendelea na maisha sehemu nyingine. Ombwe analoliacha nyuma mara nyingi huzibwa na nyoka au ndege wengine ambao ni wavivu kujenga viota. Kitu kimoja cha msingi kufahamu ni kwamba ndege ambao mayai yao yana rangi nyeupe, hupenda kujenga viota na kuyaficha ndani mayai yao. Wale ambao mayai yao yana rangi isiyo nyeupe, mayai yao huweza hata kuyataga ardhini.
No comments:
Post a Comment