Tuesday, January 3, 2012

Mandhari maridhawa ya Mullers Mountain Lodge Lushoto

Ni Moja ya Lodge maridhawa iliyopo kwenye milima ya Usambara, Wilayani Lushoto mkoani Tanga. Mullers Lodge ipo takriban kilometa 16 toka lushoto mjini. Ipo kwenye njia inayoelekea shule maarufu ya Kifungilo Girls huko Lushoto. Ni kiota mwanana kwa mapumziko hasa kwa wale wanaotafuta utulivu asilia na hali nzuri ya hewa. Picha juu ni jengo kuu la Mullers Lodge ambapo ndani kuna restaurant na sehemu ya vinywaji (ya ndani).
Moja ya vyumba vya kulala wageni.

Hii ni sehemu ya mapumziko ambayo ipo nje. Pembeni kuna sehemu ya kuotea moto kwa wale watakaohitaji nishati hiyo hususan kipindi cha baridi.


Vyumba vya lodge hii vimejengwa katika mteremko wa kilima hiki na kutoa mandhari mwanana pamoja na hewa nzuri kwa wakazi wa lodge. Ni sehemu ambayo mandhari asilia ya eneo hili imebakishwa kwa kiasi kikubwa.

Hii ni maabara ya nje iliyopo pembeni mwa jengo kuu la Mullers. Kama ukijisikia baridi unaweza hamia maabara ya ndani na kuendelea na moja moto moja baridi.

Kulia ni chumba kilichojengwa kwa mfumo wa combo - vyumba viwili pamoja na sebule moja kati. Muhimu kwa wageni wanaosafiri makundi ambao wangependa kukaa pamoja au wana familia.

Hii miti huku ndio kwao. ni kama ilivyo mi-arobaini hapa dar na sehemu nyingine za pwani

Asubuhi na mida mingine (kipindi cha baridi) utakuta umewekewa shehena yako ya magogo kadhaa kwa ajili ya kuwasha kwenye sehemu ya kuotea moto kwenye chumba chako. Huduma hii huwepo hasa kipindi cha Baridi. Tembelea tovuti yao kwa kubofya hapa ili uweze kujionea mambo mengi zaidi kuhusu hoteli hii ya kipekee ya huko Lushoto. Timu ya Tembea Tanzania ilibahatika kuitembelea hoteli hii mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana. Stay tuned kwa picha zaidi za safari hii...

No comments:

Post a Comment