Tuesday, January 3, 2012

Ingizo jipya ndani ya DSM ZOO

Katika hali ya kuboresha na kunogesha mambo ndani ya Dar Es Salaam Zoo, uongozi wa zoo hii hivi karibuni uliongeza aina mpya wanyama ndani ya hii zoo. Nao si wengine bali ni Nyati-Maji (Water Buffalo).

Ni wanyama ambao hupenda kutumia muda mwingi ndani ya maji hasa pale wasipokuwa wanakula. Hupatikana kwa wingi bara la Asia lakini pia wanamudu mazingira ya huku kwetu. Picha kwa hisani ya Mdau Salim Hassan wa DSM Zoo.

1 comment:

  1. je ni endelevu kwa kizazi cha baadae?

    ReplyDelete