Tuliwakuta sharubu hawa wakiuchapa usingizi pembezoni mwa ziwa Nzerekela. Walikuwa majike wawili wakiwa wamelala chini ya palm tree. Tulipofika getini tulipewa dondoo ya uwepo wa hawa sharubu na hivyo mipango ya mizunguko yetu ilikuwa ni lazima tupite maeneo haya ili tuweze kuwaona.
Licha ya magari kadhaa kupita hapo na kukaa kwa muda, sharubu hawa hawakuwa na shaka na waliendelea kuuchapa usingizi bila wasiwasi.
Baadae mmoja aliamka baada ya kenge mmoja kuibuka toka machakani na kupita karibu yao.
Hawa walikuwa ni sharubu wa kwanza kuwaona siku hii baada ya kuingia ndani ya Pori la Akiba la Selous. Ilikuwa rahisi kwetu kuwapata kwani tulishadokezwa na madereva waliotutangulia kuhusu uwepo wao sharubu hawa eneo hili. Ni ushirikiano wa kipekee ambao unakuwepo baina ya madereva wa watalii ndani ya hifadhi zetu. Kwa bahati nzuri, sharubu hawa walibaki eneo hili kwa kipindi kirefu.
Sharubu wanakuwa na tabia ya kubakia eneo moja kwa muda mrefu kipindi cha mchana kutokana na ukweli ya kwamba wao hufanya mawindo yao mida ya usiku. Jua linapochomoza, hutafuta kivuli na kuuchapa usingizi. Ndio maana mara nyingi wageni huwakuta sharubu wakiwa ktk mapozi ya kulala. Hali ni tofauti kwa wanyama kama mchakamchaka, wa chini au bwana afya. baadhi yao huwa na mishe mishe nyingi mida ya mchana hivyo usitegemee kuwakuta sehemu moja ukiwa porini.

No comments:
Post a Comment