Tuesday, November 15, 2011

Ndio territory yake iliyobakia

Tulimkuta huyu kiboko akiwa amejitosa kwenye dimbwi dogo lililobakia baada ya sehemu kubwa ya ziwa Nzerekela kukauka. Hii ni kutokana na kupungua kwa kina cha maji kwenye mto Rufiji. Nilidokezwa ya kwamba kiboko huyu hapa ndio territory yake iliyobakia na kumlazimu kuendelea kubaki hapo. akienda kwengine watamtoa spidi na atalazimika kuingia kwenye mpambano na dume anayemiliki eneo atakalovamia ili aweze kupewa hifadhi.

Alikuwa ni kiboko mkubwa.

Kwa kawaida sehemu aliyo kiboko huyo na hata sehemu aliyosimama huyo twiga huwa ipo ndani ya Ziwa nzerekela. Kipindi cha kiangazi eneo hili hujulikana kama kidongo cheusi.

No comments:

Post a Comment