Sunday, October 30, 2011

Toka Campsite kuelekea Geti la Mtemere

Kwa wewe ambae utakuwa umelala ktk moja ya campsites zilizopo nje ya Pori la akiba (Mloka), unakuwa una kiji-safari cha kama kilometa 5-6 hivi mpaka kufika geti la Mtemere la kuingilia ndani ya Selous GR. Campsites nyingi zimejengwa pembezoni mwa mto Rufiji, zikiwa zimefuatana. Picha juu ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Hippo camp na barabara kuu inayoelekea Mtemere Gate. Japo mpaka wa hifadhi upo kilometa kadhaa toka hapa, wanyama kama Tembo, Swala, Viboko, Nyati na wengineo wanakuwepo maeneo haya nje ya ya hifadhi. Ushahidi wa haya huonekana kwa nyayo na vinyesi vyao. Ndio maana baadhi ya wageni huamua kufanya game/bush walk huku nje kwani napo kuna kuwa na fursa ya kuona vitu adimu.

Hii ndio barabara inayoelekea Getini, Mtemere. Na ndio hii itakayokurudisha Kibiti.
Hapa ndio border, ukiendelea mbele unakuwa unaingia ndani ya eneo la pori la akiba la Selous.

Zingatia maelezo umbali mpaka lilipo geti lenyewe (ofisi) ni kama Kilometa 3 unusu hivi

Hapa ni ndani ya Pori la akiba la Selous lakini kabla ya kufika getini. Kulia kwa barabara hii kuna uwanja mdogo wa ndege wa mtemere.

No comments:

Post a Comment