Sunday, August 28, 2011

Mtemere airstrip - Selous GR

katika kijiji cha Mloka ndipo unapokutana na geti la Mloka, lango ambalo linaweza kukuingiza ndani ya pori la akiba la Selous. Sambamba na ofisi za maofisa wa maliasili, pembezoni kuna uwanja mdogo wa ndege ujulikanao kama Mtemere air strip. Ni moja ya viwanja kadhaa vya ndege vilivyomo ndani ya pori la Selous. Vingine ni Matambwe-mahali ambako yapo makao makuu ya wahifadhi wa pori la akiba Selous, Behobeho n.k. Hapa hutua ndege zilizokodishwa - chartered flights. Pia kuna baadhi ya mashirika ya ndege ya hapa nyumbani ambayo yanakuwa na safari za kila siku - scheduled flights - kwenda mtemere. Picha juu ni Ndege mali ya kampuni ya ZanAir ikitua Mtemere.

Kutokana na ukubwa wa pori la Selous, baadhi ya mashirika ya ndege yanakuwa na ndege zinazotua katika viwanja vingine pia ndani ya Selous ili kuweza kuwafikisha haraka wageni kule wanakoelekea. Kwa kukufahamisha tu, umbali wa barabara toka mtemere mpaka matambwe ni karibu kilometa 75. hapo ndege ya ZanAir ikisogea sehemu ya kushushia abiria na kupakia wengine.
Waliofika wanashuka na wanaoondoka wanapanda, ndio mpango unaoonekana kuendelea..

Vinwanja hivi huwa havina barabara ya lami kama ambavyo inavyoonekana katika mtundiko huu. Ndege ndogo na zile saizi ya kati ndizo zinafanya safari zake huko. Picha za mtundiko zimedodonshwa na Mdau Stephen wa Kima Safaris aliyekuwa Selous GR hivi karibuni. Bofya hapa kuona mitundiko mingine yaawali ya TembeaTZ.. 2009 na 2010

No comments:

Post a Comment