Thursday, June 9, 2011

Utalii wa tiba

Kuibuka kwa Babu wa Samunge kuliibua dhana mpya ya utalii hapa nchini kwetu, Utalii wa tiba. Hali iliyopeleka kuibuka kwa mambo mengi ikiwemo matumizi ya helkopta kwa wale waliokuwa wanataka kwenda kupata tiba kwa babu haraka. Nilipokuwa Arusha niliziona Helikopta mbili zikiwa zimeegeshwa ktk Uwanja wa ndege wa Arusha ambako ndiko safari za helikopta huanzia. Nilidokezwa ya kwamba kipindi kulipokuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa kwenda samunge, Helikopta zilikuwa zaidi ya nne na zote zilikuwa zikifanya safari zaidi ya mbili kupeleka wageni kwa babu.

Hii ni mojawapo ya helikopta ambayo ipo Arusha kwa safari za kwenda Samunge na matumizi mengineyo kadri mteja atavyohitaji.

Hapa helikopta hii ikipakia abiria wake tayari kwenda Samunge.

safari ya kwenda Samunge imeiva na hapo Helikopta ikichanja mbuga. Safari za helikopta huchukua saa moja kwenda Samunge tokea Arusha.
Nikiwa maeneo ya Airport nilimsikia rubani wa moja ya hizi helikopta akisema ya kwamba sasa hivi biashara ya Samunge imedorora kiasi ya kwamba kampuni yake inaweza kuirudisha helikopta yao nyumbani. Helikopta hii ni ya kampuni toka nje ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment