Thursday, June 9, 2011

Karibu fair 2011 - Burudani zilikuwepo kedekede..

Ktk maonesho ya mwaka huu ya Karibu, kulikuwa na burudani mbalimbali ambazo ziliandaliwa kwa wageni waliotembelea viwanja vya maonesho. Waliokuwa na shauku ya kupanda ngamia, ngamia walikuwepo.

Kampuni ya ulinzi ya KK security nayo ilifanya onyesho la mbwa wake wanaotumiwa ktk shughuli mbalimbali za ulinzi.

Sarakasi zilikuwepo pia

Mwanamuziki Ndanda Kossovo "kichaa" (tatu kulia) alikuwepo na kundi lake la watoto wa Tembo ambao kwa pamoja waliwapagawisha wageni waliotembelea banda la TBL kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro lager.

Ndanda Kossovo (katikati) na vijana Watoto wa tembo wakiwajibika. Arusha ndio yamekuwa makazi ya mwanamuziki huyu tokea aliporejea tena nchini

No comments:

Post a Comment