Friday, June 3, 2011

Mhe Nyalandu azindua rasmi Karibu fair 2011

Mhe Lazaro Nyalandu, Naibu waziri wa viwanda na biashara leo mchana amefungua rasmi maonesho ya Karibu fair 2011 kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda. Baada ya kufika uwanja wa maonesho, Mhe Nyalandu alilakiwa na mwenyeji wake Mhe Mustapha Akunaay ambae ni Mwenyekiti wa TATOTZ na mjumbe wa bodi wa Karibu fair. alizungushwa katika mabanda ya makampuni mbalimbali zinazoshiriki maonesho ya mwaka huu.

Hapa akipata maelezo toka kwa dada Grace ktk banda maalum la Karibu fair linalotumika kuratibu shughuli mbalimbali hapa uwanja wa maonesho.

Akiwa ktk banda la Mount Meru Hotel

Hapa alipotembelea banda la Tanga regional tourism Association

alipata fursa ya kupata picha ya kumbukumbu na viongozi wa TATOTZ

Picha ya pamoja na wadau wa banda la Wizara ya maliasili na utalii pamoja na TTB

No comments:

Post a Comment