Friday, June 3, 2011

Manyara Ranch Conservancy

Manyara Ranch Conservancy ni eneo lenye takriban hekta 35000 ambalo lipo kati ya hifadhi za Manyara na Tarangire. Ni eneo ambalo lilianzishwa kwa lengo la kuhifadhi ushorobo (corridors) ambazo hutumiwa na wanyama wanaohama kati ya hifadhi za Manyara na Tarangire. Kampuni ya Manyara Ranch conservancy ndio inayosimama na kuendesha shughuli za utalii katika eneo hili. Picha juu inaonyesha ramani ya eneo ambalo Manyara Ranch ipo. linaanzia kilometa chache baada ya njia panda ya makuyuni.

wageni wanaotembealea Manyara Ranch hupata fursa ya kufanya game safari za mchana na za usiku pia. sambamba na hizo walking safaris zipo pia. Picha juu ni picha zinazoonyesha mambo mbalimbali ambayo wageni wanaweza kupata

Tembelea Tovuti yao kupata taarifa zaidi
www.manyararanch.com
Bofya hapa kwa picha zaidi toka Manyara Ranch

No comments:

Post a Comment