Baada ya sehemu nyingi hapa nchini kupata mvua za kutosha (japo ktk vipindi tofauti) maeneo mengi yanaonekana kutawaliwa na rangi ya kijani kuashiria hali ya uoto kuwa nzuri. Mtundiko huu una taswira kadhaa nilizoweza kupiga hivi karibuni nikiwa njiani kuelekea Arusha. Picha juu ni kwenye mteremko wa Kuelekea Daraja la mto Wami.
Ukivuka daraja la mto wami na kumaliza mwinuko wa bonde la mtu huo unakutana na kijiji kijulikanacho kama Mandera. Hapo ndipo kuna njia panda itakayokufikisha hifadhi ya taifa ya Saadani. Kwa yule anaeelekea Tanga, atakata kulia. Picha juu ni kibao kinachoonyesha njia hiyo kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Saadani huko Bagamoyo. Saadani ni Hifadhi ya taifa pekee afrika mashariki ambayo inapakana na Bahari ya hindi. Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu Saadani NP.
Korogwe, karibu kabisa na Highway restaurant. Milima unayoiona kwa mbali ni milima ya Usambara. Huko ndipo ilipo Lushoto
wale wanaolekea Lushoto wakifika Mombo wanashika njia unayoiona hapo juu kuelekea Maeneo kadhaa yaliyopo huko juu ukiwemo Lushoto
Nilipokuwa nakaribia kufika Himo njiapanda nilipoteza matumaini ya kuona kilele cha Mlima Kilimanjaro siku hii kwani mlima ulizungukwa na mawingu mwengi.
Mambo yaligeuka nilipokuwa nakaribia kufika Moshi mjini ambapo kuna mahali Mlima Kilimanjaro ulikuwa Umeachia. Sikusita kuunasa kwenye kemera yangu. Muda mfupi baadae mawingu yaliuzingira na kilelel cha Kibo kikapotea kwenye mawingu hayo. Nilipoingia Moshi mjini Mlima Kilele cha Kibo hakikuwa kikionekana kabisa
No comments:
Post a Comment