Wednesday, June 22, 2011

Hii ndio gharama ya kuwa na uwezo wa kusaga mifupa...

Si jambo la ajabu kumkuta fisi aka Bwana afya akiwa amejitosa kwenye dimbwi la maji au tope kabisa kama anavyoonekana huyu. Ni tabia ya kawaida na mara nyingi huwa ni bwana afya aliyekula na kushiba.

Kama anavyojulikana, fisi haachi kitu kwenye mlo. Ataanza kula nyama na nyama ikiisha atahamia kwenye sehemu nyingine za mnyama - Ngozi na mifupa ya sehemu mbalimbali. Mungu amemjalia bwana afya uwezo wa kuweza kutafuna na kuvunja mifupa na baada ya kuingia tumboni mwake fisi ana acid kali zinazoweza kusaga mifupa aliyomeza. Mchakato wa kumeng'enya mifupa na hizo zaga-zaga nyingine alizokula huzalisha joto kali mno ambalo fisi asipotafuta namna ya kukabiliana nalo anaweza kupata madhara ktk viungo vyake vya ndani ya mwili - internal organ failure.
Moja ya namna ya kupambana na joto hilo ni kujitosa kwenye tope. katika maeneo yenye ukame au kipindi cha kiangazi, fisi hupambana na joto hili kwa kujificha kwenye vichaka au vivuli vya miti au mapangoni. Kuzalishwa kwa joto kali wakati wa digestion kunaelezwa pia ni moja ya sababu inayompelekea bwana afya kupenda kutafuta chakula usiku kipindi ambacho hakuna joto na hivyo kumrahisishia uwezo wa kupambana na joto hilo. Endapo atapata msosi wakati wa mchana, basi atalazimika kutafuta hifadhi kwenye maji, tombe au kivuli pindi digestion process ikianza kushika kasi.

(picha | Mdau GBM - Ngorongoro crater)

1 comment: