Thursday, May 19, 2011

Ungeweza kuwa karibu na tembo kiasi hiki?

kwa muonekano wa taswira hii, ni dhahiri ya kwamba mpiga picha alikuwa yumo ndani ya gari. Kuna mtu aliwahi kuiona hii picha na akatamka bayana ya kwamba yeye asingeweza kustahimili kuwa karibu na Tembo kiasi hiki. Sikumshangaa sana kwani wanadamu twatofautiana kwa mengi ikiwemo uwezo wetu wa kuhimili vishindo kama hivi. Licha ya kwamba hawa wanyama wanaitwa wanyama wa porini, lakini zipo taarifa za wanyama hawa kutoka nje ya mapori yao na kuja kuingia ktk maeneo ya makazi ya wanadamu. Hali ambayo inaweza kukufanya ukutane nae uso kwa uso wakati wewe haujajiandaa na ukiwa nje ya gari au nyumba. Ktk hali kama hii, jambo moja ndilo linaweza kutofautisha kati ya wewe kuendelea kuishi au kujeruhiwa na mnyama yule - uelewa wa tabia na mwenendo wa wanyama hawa.

Zamani kidogo niliwahi kukutana na mdau na mweledi mmoja wa mambo ya porini na akanimbia ya kwamba wanyama wa porini huwaogopa wanadamu. Ni pale tu mwanadamu anapoonyesha dalili za udhaifu ndipo mnyama huamua kumshambulia. Ndio maana akaniambia watu wanaweza wakalala ktk mahema madogo ndani ya hifadhi na usisikie habari ya mtu kushambuliwa au kuvamiwa na mnyama akiwa ndani ya hema. Hii inatokana na ukweli wa kwamba mnyama yule anapigwa na butwaa kwa muonekano wa hema lile na kisha anabaki haelewi nini afanye. Kwa siku ile (miaka kama 7 iliyopita) nilifanya kubaili yaishe lakini baadae nilipekua vitabu kadhaa vinavyohusu tabia za wanyama (hususan wa porini) na kupata maandishi yaliyonithibitishia hili.

Kukimbia, Kuhamaki na kuanza kupiga mayowe, kuonyesha hali ya kuchoka na kudhoofika - kuchechemea ni baadhi ya viasharia ambavyo mnyama huviangalia kabla ya kufanya uamuzi wa kushambulia au kukimbia kunusuru maisha yake. Hili la kupiga mayowe kwa mnyama kama Masikio ndio hatari zaidi.

No comments:

Post a Comment