Thursday, May 19, 2011

Ni Kinga dhidi ya wadudu wanaomkwaza...

Tembo na wanyama wengine hutumia vumbi au matope kama kinga dhidi ya wadudu wanaowatambaa kwenye ngozi yao na kuwakera. Anapojimwagia vumbi mwili (kama anvyoonekana ktk picha ya juu), wadudu ambao wameshamdandia hufa kutokana na kukosa hewa au mazingira ya maisha kuwa mabaya juu ya ngozi yake. Baada ya muda, tembo hutafuta bwawa la maji au mto na kisha kujiloweka ili kuondoa udongo/tope lililopo juu yake sambamba na wadudu walionaswa na kufia humo.

(picha | Mdau Aenea wa Tanzania Giraffe Safaris)

No comments:

Post a Comment