Wednesday, May 18, 2011

Mji wa Moshi huonekana tokea Maundi Crater

Uwapo kwenye crater rim ya Maundi crater katika siku isiyokuwa na mawingu au mvua, unaweza kuuona mji wa moshi ukiwa chini yako. Awali nilipoelezwa hili ilinichukua muda mwingi kuamini kwani akilini mwangu safari ya kufika Marangu gate ilinifanya nijihisi nimeenda mbali sana na mji wa Moshi. Ukweli ni kwamba nilikuwa nimeuzunguka mji wa Moshi na kuja kutokea nyuma ya mji huu.
Kwa siku hii, mvua na mawingu vilizuia uwezo wetu wa kuona mbali na kuthibitisha zaidi. Kuna sehemu unapokuwa njiani hata Mji wa Arusha huwa unakuwa unaoneka mida ya Usiku (taa)
(Picha | Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment