Tuesday, April 19, 2011

Taswira za Mandara hut (2720m ASL) - Marangu route

Muonekano wa Mandara point baada ya kuchomoka ktk msitu ambako ndio kuna njia inayokufikisha hapo.

Picha hii nimeipiga nikiwa nimesimama mbele ya banda la kupatia maakuli - mesi. mabanda madago unayoyaona ni mabanda kwa ajili ya kulala wageni wanaopanda mlima. Banda moja wanalala watu nane(8).

Picha hii nimeipiga nikiwa nimesimama mbele ya banda la maakuli lakini nikiwa nimegeukia upande tofauti na picha ya awali (kushoto). Banda kubwa (kulia) ni ofisi/reception ya Mandara point. Ndio banda ambalo linaonekana ktk picha ya kwanza ya mtundiko huu. Mabanda mengine ni kwa ajili ya kufikia wapagazi/porters na wasindikizaji na malazi kwa ajili ya wahifadhi wanaokuwa zamu Mandara hut.

Mabanda ya kufikia wageni yakionekana kwa angle tofauti. hapa nilikuwa nimesimama karibu na banda la mapokezi

Wadau wakichomoza toka msituni na kuingia rasmi Mandara point

baadhi ya mabanda yanayotumiwa na guides na porters wakiwa Mandara.

Nikiwa mbele ya banda la mapokezi.

Banda kubwa unaloliona ndio mesi ya wageni wote wanaofika Mandara hut. Hapo na sisi ndipo tulipopata vitafunwa vyetu tulivyobeba, huku chakula chako unakuja nacho. Njaa ilitukamata sio mchezo. Mbele ni mdau Hussein aliyenisindikiza toka Arusha mpaka huku. Kundi la watu linaloonekana mbele ya mesi ni wageni toka nje ya nchi ambao walikuwa wameingia mandara muda huo. walikuwa wageni kama 20 hivi. Hapo walikuwa wanapewa utaratibu na mpango wao baada ya kuwasili Mandara salama.

No comments:

Post a Comment