Tuesday, April 19, 2011

Kituo kinachofuata ni Horombo

Ukifika Mandara hut utakutana na kibao kinachokupa maelezo ya kituo kinachofuata kuelekea Uhuru peak kupitia njia ya Marangu. Safari ya kutoka Marangu gate mpaka Mandara hut ni ya umbali wa takriban kilometa 8.3. hivyo kwa safari ya kwenda na kurudi (day trip) ni mwendo wa karibu kilometa 16.6.

Horombo ipo umbali wa Kilometa 11.7 tokea Mandara hut. Kwa makadirio ya wahifadhi safari hii inaweza kukuchukua masaa 5 mpaka sita. hii inategemeana na stamina ya mtu na maandalizi aliyofanya. Kiukweli kuupanda Mlima kilimanjaro kwa lengo na nia ya kufika Uhuru ni jambo linalohitaji maandalizi ya ki mwili na kiakili.
Mgeni anapofika Mandara hut hulazimika kulala Mandara hut na kuendelea na safari yake kuelekea Horombo siku inayofuata. Utaratibu huu umewekwa ili kuuruhusu mwili wa mpandaji uweze kuanza kuzoea hali ya hewa ya mlimani. Pia, kwa jinsi umbali ulivyo, mgeni akiamua kuunganisha anaweza jikuta giza linamkuta ukiwa bado hujafika Horombo. Jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa wapandaji. kwa sehemu kubwa ya safari ya kuupanda mlima, wageni hawaruhusiwi kutembea usiku. Ni hatua ya mwishoa kabisa (kuelekea Uhuru point) ndipo wageni huanza safari yao alfajiri na mapema.

Mgeni awapo Mandara anaweza fanya safari mpaka eneo lijulikanalo kama Maundi crater. Hii ni sehemu ambayo wanaofanya day trip wanaweza kwenda pia. ni mwendo wa takriban dakika 15 toka Mandara hut. Njia unayoiona (invyoonyeshwa na vibao) ndio inayokwenda Maundi crater, Horombo na kwengineko kuelekea Uhuru point. Kwa wale wanakuwa wanaendelea na safari kuelekea juu, safari ya maundi crater hutumika kuuzoesha mwili - acclimatisation - mgeni anapowasili Mandara hut. Siku hii na sisi tulichapa mwendo mpaka Maundi crater.

1 comment:

  1. Nimefuatilia posts za safari yako ya kupanda mlima Kilimanjaro. nahisi kama nami nimeshapanda mlima kilimanjaro maana umeelezea vizuri na kunifungua macho yangu. mengi uliyoyaelezea kwangu yalikuwa mageni na wala sikuwahi kuhoji

    Mdau,
    Dodoma

    ReplyDelete