Sunday, April 17, 2011

Taka ngumu unashuka nazo..

katika jitihada za kuhakikisha kuwa mazingira ndani ya hifadhi yanakuwa salama na endelevu, wahifadhi wa mlima Kilimanjaro wameweka utaratibu ambao unamlazimu mpandaji kushuka na taka ngumu zote ambazo ameingia nazo ktk hifadhi. hii inamaanisha, taka zozote unazozizalisha ktk safari yako unatakiwa kuzibeba na uje kuzitupa unapofika mwisho wa safari. Taratibu hii haihusu taka za mwilini.
Utaratibu huu umewekwa ili kuondoa ulazima wa kuwa na sehemu za kutupia na kuharibu taka ngumu ndani ya hifadhi. nilidokezwa ya kwamba awali wapandaji walikuwa wakitupa taka ktk vituo vya kupumzikia na hapo zilikuwa zikikusanywa na kutupwa pamoja. utaratibu huu ulikuja kugundulika baadae ulikuwa unakaribisha wanyama hatarishi katika maeneo taka hizo zilipokuwa zinatupwa.
Usafi ni jambo ambalo linasimamiwa kikamilifu ktk route zito kuelekea uhuru point. jitahidi kadri uwezavyo kuonyesha ushirikiano kikamilifu nje ya hapo utalimwa fine na wahifadhi.
Picha juu ni baadhi ya taka ngumu nilizozilisha siku nilipofanya day trip. nilishuka nazo na kuja kuzitupa marangu gate wakati wa kutoka

No comments:

Post a Comment