Monday, April 4, 2011

Njia za Mlimani - Marangu route

Ukisikia mtu kapanda mlima Kilimanjaro kwa kupitia njia ya Marangu, basi tambua ya kwamba atakuwa amepita moja ya sehemu zinazoonekana ktk mtundiko huu. Ni baadhi ya maeneo ambayo nilipita kuelekea Mandara hut. Eneo kati ya Marangu gate na Mandara hut ni msitu hivyo sehemu kubwa safari hii inakuwa ni sawa na safari ya miguu ktk msitu

Kutokana na eneo hili kuwa la uoto wa msitu (alpine forest), wahifadhi wakaamua kuweka njia tofauti kwa ajili ya wapagazi ili wasipate shida kupanda na mizigo yao. Sehemu kubwa ya kipande hiki, wapagazi na mizigo yao wanatumia barabara yao maalum ambayo haina vikwazo vya miti au matawi yaliyoshuka chini. Huku wageni mnakuwa mnachapa mwendo na msindikizaji wenu


Siku hii kulikuwa na mvua nyingi iliyopelekea uwepo wa ukungu sehemu kubwa ya safari kuelekea mandara hut

Ukifika sehemu kama hizi nguvu ndio huwa zinaweza zikakuishia, sio kilima kirefu lakini unakuwa hoi. Unachotakiwa kufanya ni kutembea taratibu bila kujilazimisha.


No comments:

Post a Comment