Thursday, April 7, 2011

Kisambioni - Marangu Route

Kisambioni ni neno la kichaga lenye maana ya mahali pa kufanyia mabadiliko. Mathalan, ni mahali ambapo mtu anaetoka shambani hufika na kunawa na kuondoa hali ya kazi ya shambani na kujiandaa kuingia uraiani. Ktk route ya Marangu, kuna eneo limepewa jina la Kisambioni. hii inatokana na maelezo ya kwamba wapagazi wa awali walikuwa wanatumia eneo hilo kubadili kabla ya kuingia uraiani. sasa hivi Kisambioni ni eneo ambalo wapandaji husimama na kula chakula. Kisambioni ipo katikati ya Marangu gate na Mandara hut, hali ambayo imapafanya pajulikane pia kama nusu-njia.

Tangazo ambalo linawasisitiza wageni kutumia njia mahususi kwa ajili yao na kuachana na njia ambayo imetengwa kwa ajili ya wapagazi na wahifadhi

Hii ndio njia ambayo inatumiwa na wapagazi kwa sehemu kubwa ya safari kati ya Marangu gate na Mandara hut. Hii inatokana na hali ya uoto wa eneo hili - msitu. Wahifadhi waliamua kuweka njia mbadala kwa ajili ya wapagazi na mizigo yao. Mbele ya safari, muda mfupi kabla ya kufika Mandara Hut njia hizi huungana na kuwa moja. Njia hii pia hutumika kwenye dharura. wapandaji wanaokumbana na changamoto za kiafya wakiwa safarani hushushwa chini kupitia njia hii aidha kwa kutumia magari ya KINAPA au toli toli maalumu kwa kubebea wagonjwa. mtu anapokumbwa na tatizo lolote la kiafya anapokuwa anapanda mlima, jambo la muhimu ni kuanza kumshusha chini ambako kuna oksijeni ya kutosha. matatizo mengi ya kiafya wanayokumbana nayo wapandaji hutokana na mwili kushindwa kuhimili hali upungufu wa hewa ya oksijeni huko juu.

Kisambioni ni picnic site pia. Wapandaji huweza kusimama na kupata msosi kabla ya kuendelea na safari kuelekea Mandara Hut.


Mie nikiwa Kisambioni.

2 comments:

  1. U real do a great job kaka,,,big up sana,,blog yako inatufundisha vitu vingi sana vinavyohusu maliasili zetu ambavyo hatuvifahamu...endelea hvyhvy tupo pamoja!
    Mdau namba 1 wa tembea TZ
    Moscow-Russia

    ReplyDelete
  2. thanks Mdau kwa kutuelezea issue za wanyama wa nchi yetu.

    ReplyDelete