Nilipokuwa mdogo niliwahi kukuta mahali pameandikwa Hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro. mwanzoni nilihisi ni hifadhi ambayo ipo mbali na mlima. Nilipata fikra hizi kutoka na ukweli wa kwamba kipindi hicho neno hifadhi ya Taifa liliambatana na uwepo wa wanyama wakali na wakubwa. Lilinichanganya kutokana na ukweli ya kwamba nilifahamu ya kuwa kwenye hifadhi za taifa ni lazima kuna wanyama wakali - Simba, chui, faru, tembo... Nikawa nakosa namna ya kujiridhisha inawezekana vipi waoupanda mlima kuupanda wakati kuna wanyama hawa? nilipatwa na maswali mengi ambayo nashukuru siku moja nilibahatika kumpata mwelewa aliyenielewesha vyema. Ni fikra ambazo nilizipata utotoni ambazo yawezekana kuna watoto wengi wanazo au hata watu wazima pia
KINAPA ni hifadhi ambayo iliyoundwa mahsusi kulinda na kuhifadhi mazingira yanayouzunguka mlima wetu wa Kilimanjaro. Hii hufanya mlima kuwa chini ya uangalizi mzuri dhidi ya uhalifu na uharibifu wa namna yoyote ile
Route zote zinapita maeneo ambayo hayana wanyama wakali. ktk safari yetu tulikutana na tumbili kadhaa (white and black colobus monkeys) ambao walikuwa wakiendelea na shughuli zao.
No comments:
Post a Comment