Friday, April 1, 2011

Hans Meyer na Lauwo


Inaelezwa ya kwamba Hans Meyere ndiye eliyekuwa mzungu wa kwanza kuukwea mlima kilimanjaro mpaka Kileleni ambapo Mtanzania kwa jina la Lauwo ndiye alikuwa guide wake. Ukiachia hao wawili, kulikuwa na wapagazi wengine kadhaa waliowasidia katika safari yao. Hans Meyer alifanya majaribio mara mbili jaribio la kwanza likiwa ni mwaka 1887. hakufanikiwa kufika kileleni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa hali mbaya ya hewa aliyokutana nayo huko juu na yeye kukosa vifaa vya kukabiliana nayo. Jaribio la mwaka 1889 ndilo lililomwezesha kufika kileleni mnano tarehe 5 October 1889.

No comments:

Post a Comment