Baadhi ya jamii zinazoishi maeneo ambayo ni maarufu kwa utalii hapa nchini yameweka utaratibu unaotoa fursa kwa wageni kujifunza mila na tamaduni za jamii hiyo. Tunaweza dhani kuwa cultural tourism unawafaa wageni toka nje lakini hata kwa sisi wanyumbani tuna mengi ya kujifunza kwa jamii mbalimbali tunazoishi nazo. Haina haja ya kufanya safari maalum lakini kila unapofika mahali ambako jamii fulani inapaita nyumbani, kuwa msikivu na mdadisi na utaweza kujua mengi kuhusu jamii ile. Mwisho wa siku, yale machache unayoyapata huko yanaweza kuwa na msaada kwako sehemu ambayo hata hukutegemea. Hii ilikuwa ni ngoma ya kabila la wamasai ambayo ilikuwa imeandaliwa mahsusi kwa ajili ya wageni waliwatembelea ktk kituo chao cha utamaduni Mdau Aenea ta Tanzania Giraffe Safaris nae hakuwa nyuma baada ya mzuka wa ngoma ya kimasai kumpanda. Bila ya kujijua alijikuta akiunga tela
No comments:
Post a Comment