Sunday, March 6, 2011

Mchungaji wa Loliondo - Anaweza kuifanya Tz kuwa kivutio kwa wageni?

magazeti kadhaa ya hapa nyumbani hii leo yamebeba habari ya Mchungaji mstaafu wa huko Loliondo ambaye anatoa dawa inayotibu magonjwa kadha wa kadha yakiwemo Kisukari, Ukimwi, shinikizo la damu na kadhalika. Mji wa Arusha umekuwa ukipata wageni lukuki toka ndani na nje ya nchi kwenda huko. Wadau kadhaa ambao Tembeatz imeongea nao toka Arusha wamebaini ukweli wa habari hizi na wengine wamethibitisha kusikia kwa jamaa zao waliopona baadhi ya magonjwa yaliowafanya wafuate tiba kwa Mchungaji huyo. Soma zaidi habari ktk tovuti ya Gazeti la Mwananchi

Habari hii inaweza sababisha ongezeko la wageni wanaokuja kuitembelea nchi yetu kwa lengo la kupata tiba na kuliongezea taifa kipato?

No comments:

Post a Comment