Thursday, March 24, 2011

..Maisha yanakuwa yanaendelea...

Licha ya kwamba ukame unakuwa unatawala, lakini maisha huwa yanakuwa yanaendelea ndani ya crater japo ktk hali tofuati na kawaida. Kundi la nyumbu likiwa limetulia pembezoni mwa ziwa Magadi ndani ya crater. Nyumbu unaowakuta Ngorongoro nao hushiriki ktk ile great migration sambamba na wenzao wa Serengeti. japo sio wote huhama.

Rangi ya kahawia hurahisa mawindo ya sharubu kwa kuwa inarandana na rangi ya ngozi zao. hawa walikuwa wamejificha pembezoni mwa ziwa. lilikuwa ni kundi la Sharubu jike na watoto kadhaa.

Taswira hii imepigwa tokea picnic site ya ngoitoktok.

Wazee wa kazi hawakuwa mbali na majike na watoto wao. nao walikuwa wamefanya camouflege nzuri kwenye nyasi kavu.

Masikio nao wakijapita nyasi zinazipatikana ktk maeneo yenye chemchem na miti kadhaa ndani ya crater. mfumo wa maisha kwenye crater hubadilika kutokana na hali na upatikanaji wa chakula ambo hutegemea hali ya hewa kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment