Tuesday, March 22, 2011

Karibu Travel & Tourism Fair - Flashback to 2008

Tokea mwaka 2000, Jiji la Arusha limekuwa likihodhi maonesho mahususi kwa sekta ya utalii hapa nchini yajulikanayo kama Karibu Travel & Tourism Fair (wengi huzoea kuyaita Karibu Fair kwa kifupi). Maonesho haya huwaleta wadau wa kada mbalimbali ktk sekta ya utalii kuja kunadi shughuli zao kwa wageni na ma-agent wa makampuni ya utalii ya hapa nyumbani, Afrika mashariki na hata nje ya Afrika. Ni maonesho ambayo yamekuwa yakikua kwa ubora na kupanua wigo wa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali. Mwaka huu (2011) maonesho haya yamepangwa kufanyika tarehe 3-5 Juni, ktk viwanja vya magereza - Karibu na Arusha Airport. Mtundiko huu na mingine itakayofuatia itakuwa inakupa taswira mbalimbali za mambo yaliyojiri ktk maonesho yaliyotangulia, Kwa kuanzia tunaanza na maonesho ya mwaka 2008. Picha juu ni Lori linalomilikiwa na kampuni ya Kananga Lenye uwezo wa kubeba abiria wengi likiwa ktk Karibu Fair ya mwaka 2008.

hii ni Landrover iliyobadilishwa muundo ili kuweza kuwa na uwezo wa kubeba vifaa mbalimbali vya camping sambamba na abiria.

Wanaotengeneza bidhaa zinazotumika ktk mahoteli ya kitalii nao hutumia Karibu Fair kuonyesha bidhaa zao kwa wageni wanaotembelea maonesho haya.
hili ni gari ambalo nalo limefanyiwa mabadiliko ili liweze kubeba vifaa mbalimbali vya camping sambamba na abiria. Limepewa uwezo wa kubeba baiskeli kadhaa endapo mmiliki atafika mahali na kutaka kutembelea eneo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.


Shughuli ifanyike Arusha halafu Nyama choma isiwepo!...... Ahhh wapi, Nyama choma kwa sana...

Kunakuwa na michezo mbalimbali na burudani kwa ajili ya watoto na familia kwa ujumla.

Timu iliyofanikisha kazi ya mwaka 2008 ikipozi kwenye picha ya pamoja.
tembelea http://www.karibufair.com/ ili kujua ratiba na taratibu za maonesho ya mwaka 2011

No comments:

Post a Comment