Thursday, March 24, 2011

Kwanini watu huamua kulala kwenye mahema porini?

Mahema ni namna mojawapo ambayo mgeni anaweza kupata hifadhi anapokuwa ktk safari yake porini. Mahema yapo ya kila namna na vipimo. Yapo yenye baadhi ya vifaa na huduma kama uzipatazo ktk hoteli za kawaida na mengine ni sehemu tu ya kupumzisha ubavu wako baada ya ruka ruka za siku nzima mbugani au ktk hifadhi. Kwa wengine ni jambo la hatari mno na kwa wengine wanasema wao ni mahema kwa kwenda mbele wanapotia mguu porini. Yote kwa yote ni jambo ambalo lina mapokeo tofauti kwa wengi kila upande ukija na sababu zake lukuki. Kwa mtizamo wako, Nini kinawafanya watu waende maporini kwenye wanyama wakali na hatari za kila namna na kisha kulala kwenye mahema kama alivyolala mdau hapo juu - pembezoni mwa ziwa Natron?

Hili linakuwa na nafasi kidogo japo limefungwa pande zote

hili linachukua sura ya nyumba japo kuta zake ni canvas

Kwa mbele
Picha zote zimepigwa ktk Camp ya Moivaro huko Ziwa Natron

No comments:

Post a Comment