Siku moja mnamo mwaka 2008, Wadau kadhaa toka A town waliamua kuingia porini kwa lengo moja tu. kukutana mbali na nje ya purukushani za kila siku. Sehemu waliyoona wao inafaa kwa mtoko wa minajili hii ni pembezoni mwa Ziwa Natron lililopo kaskazini mwa mkoa wa Arusha. walipofika lake Natron walianza kwa mizunguko pembezoni mwa ziwa na baada kuja kupiga kambi ktk kambi ijulikanayo kama Lake Natron Tented Camp. Wadau hawa waliamua kulala kwenye mahema yao wenyewe ktk eneo la hii camp. Mtundiko huu unakupa baadhia ya taswira za Asubuhi baada ya usiku uliojaa shamra shamra za porini. Picha juu ni sehemu ya mahema waliyotumia kulalia usiku huo.
Siku hii kulikuwa na campers wengi. Haya ni baadhi ya mahema ya camp hiyo wakati huo (2008) . Yapo mahema ya madaraja kadha wa kadha ktk kambi hii.
No comments:
Post a Comment