Tuesday, February 22, 2011

Ukienda yalipo Majabali na vichaka........ Serengeti

Hapa tulimkuta Sharubu aliyekuwa ameshiba vilivyo akiwa kajihifadhi kwenye kivuli cha majabali haya na miti.

Sharubu mama na wanawe wakiwa wamelala juu ya mwamba uliokuwa na kivuli kuzuri cha miti iliyoota juu ya mwamba huo.

Hapa napo Sharubu jike alikuwa kahifadhi wanae kwenye mwamba

Huyu ndio alikuwa kauchapa usingizi na wala hakutaka kujionyesha sura yake tuliposogea karibu na mahali alipokuwa kapumzika.

Haikuwa rahisi kuweza kujua alikuwa ni jike au Dume, lakini kiubwa ni kwamba alikuwa ni Sharubu.

Hawa walilikimbia jua kwa kujificha china ya mti uliokuwa sambamba na hayo mawe.

Hili lilikuwa ni kundi kubwa kidogo ambalo baadhi ya sharubu walikuwa kivulini chini ya mti na wengine wakiwa mahali pa wazi sambamba na dume moja (lenye manyoya mengi). Kundi hili lilikuwa limeangusha (kuua) mnyama, hatukuweza kufanya aina ya mnyama lakini palikuwa na Tumbusi wengi wakishambulia mabaki yake. walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya Serengeti, karibu na geti la Naabi.

(Picha | Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment