Sunday, February 20, 2011

kwa mbali.. kwa chati..

Miundo mbinu iliruhusu sisi kuweza kumsogelea karibu, lakini uzoefu wa guide ulimfanya asitishe zoezi lakumsogelea baada ya kuona masikio huyu akiyatanua masikio yake kwa muda mrefu. "hii si dalili nzuri, ana hasira na anaweza kutabadilikia tukizidi kumsogelea.." alisema guide tuliyekuwa nae ktk hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Tuliishia kumuangalia tembo huyu kwa mbali na tena kwa chati maana hawa jamaa wana uwezo wa kutimua mbio na kukuvuruga ushindwe kuamini kilichotokea. Unapokuwa na wazoefu, wanakuwa wanasoma ishara za nyakati na kukwepesha hatari mapema kabla haijatokea. (Picha | Maktaba ya tembeaTz)

3 comments:

 1. Mwana big up sana kwa uwajibikaji mzuri. Nimekuwa addictive na blog yenu. Tupe majina ya kisayansi ya wanyama,miti,ndege,maua na majani pls. Mdau Uk.

  ReplyDelete
 2. Kwako Mdau wa UK,
  Tunashukuru kwa maoni yako na tutayafanyia kazi kwa mitundiko ya mbele na kuyaweka ktk mipango ya maboresho ya blog yetu.
  Tuliamua kuanza na yale majina ambayo hayapo documented popote; Sharubu=Simba, Mrefu=Twiga, Wa Juu=Chui, Wa Chini=Duma, Bwana Afya=Fisi, Masikio=Tembo, Kamba=Nyoka n.k.

  Ahsante,
  KK - Tembeatz.blogspot.com

  ReplyDelete